Waziri wa kazi wa Jordan achaguliwa kuongoza mkutano wa kimataifa wa ILO

5 Juni 2013

Waziri wa kazi na usafiri wa Jordan Dr Nidal Katamine amechaguliwa kuwa Rais wa mkutano wa 102 wa kimataifa wa shirika la kazi duniani ILO ulioanza leo na kuhitimishwa Juni 20. George Njogopa na taarifa kamili.(TAARIFA YA GEORGE)

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa kongamano hilo la kimataifa, Dk Katamine amesema kuwa miongoni vya vipaumbele ambavyo atavipa msukumo mkubwa ni pamoja na kukabiliana na hali ya kuimarisha kwa uchumi ambao kwa sasa uanz kupata nguvu tangu kutokea kwa mdodoro wa mwaka 2008, uliosababisha mataifa mengi kuyumba.

Lakini pia alizungumzia suala la ukosefu wa ajira akisema kuwa kazi kubwa iliyombele yake ni kuhakikisha kwamba unakabiliana vilivyo na tatizohiloambalo linatajwa moja ya matatizo makubwa yanayoendelea kuvuruga ustawi wa dunia kwa sasa.

Dk Katamine mwenye umri wa miaka 52 amekuwa Waziri wa Kazi waJordankuanzia mwaka 2010 na mapema mwaka huu alihamishwa kwenye wizara hiyo na kupekekwa katika wizara ya Usafirishaji ambako amehudumu mpaka wakati huu akichaguliwa kuwa rais ILC.

Anakuwa Waziri wa tatu wa Jordan aliyepitia Wizara ya Kazi kuchaguliwa kwenye wadhifa huo. Kongamanohilopia limemchagua Bwana Kamran Rahman kutokaBangladeshkuwa makama wa rais akishughulika zaidi na masuala ya ajira, huku Bi Eulogia Familia kutoka Jamhuri ya Dominican akichaguliwa la ustawi wa wafanyakazi.