Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wajasiriamali wanawake Tanzania waelezea wanavyonufaika na mpango wa UM

Wajasiriamali wanawake Tanzania waelezea wanavyonufaika na mpango wa UM

Mkutano wa kimataifa kuhusu uwiano sawa wa kijinsia katika maendeleo unaanza nchini Tanzania kesho chini ya mhimili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake, UN-WOMEN na mfuko wa maendeleo ya mitaji wa Umoja wa Mataifa, UNCDF.Mkutano huo unafanyika wakati taasisi hizo mbili kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania zimetoa mafunzo ya kuboresha bidhaa zinazotengenezwa na wanachama wa mfuko wa umoja wa udhamini wa wanawake wasindikaji wa vyakula Tanzania, TWFPT mkoani Morogoro.

Kikundi hiki husindika achari za embe, unga wa lishe na siyagi ya karanga. Mwenyekiti wa chama hicho Emmy Kiula anaeleza manufaa waliyopata na changamoto.

(SAUTI YA EMMY)

Mahojiano zaidi na EMmy Kiula yatapatikana kwenye ukurasa wetu.