Fikiri, Kula, hifadhi Mazingira; Punguza Uharibifu wa chakula

5 Juni 2013

Katika kuadhimisha siku ya mazingira duniani leo Juni Tano shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira, UNEP limeitaka “kufikiri, kula, kuhifadhi mazingira na kupunguza uharibifu wa chakula katika jamii” ikiwa ndio kauli mbiu ya mwaka huu. Flora Nducha na ripoti kamili

(RIPOTI YA FLORA NDUCHA)

 Kauli hiyo ni ya kuchagiza kila mtu kupunguza upotevu wa chakula, kwani kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo FAO kila mwaka tani Bilioni Moja nukta Tatu za chakula hupotea bure ilhali mtu mmoja kati ya watu Saba duniani hulala bila kula na watoto zaidi ya 20,000 wa umri wa chini ya miaka mitano hufa kila siku kwa njaa.

 Akitoa ujumbe maalumu kuhusu siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema teknolojia inaweza kutumika kupunguza chakula kinachopotea wakati wa mavuno hasa katika nchi zinazoendelea na hatimaye kuokoa pesa, rasilimali na kupunguza uharibifu wa mazingira na hivyo kuwa na dunia ambayo kwamo kila mtu ana chakula cha kutosha.

Tanzaniani miongoni mwa nchi zinazoendelea zinazojitahidi kupata suluhu ya kufifadhi chakula ,je hali ikoje huyu hapa naibu Katibu Mkuu wa wizara ya chakula ,kilimo na ushirika Mbogo Futakamba

(SAUTI YA MBOGO FUTAKAMBA)