Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM kuwarejesha wahamiaji waethiopia kwa hiari yao

IOM kuwarejesha wahamiaji waethiopia kwa hiari yao

Kila mwaka maelfu ya waethiopia huvuka mipaka kuelekea, Saudia, Yemen na nchi za ugaibuni kutafuta ajira lakini safari yao mara nyingi hukatizwa  kwa sababu ya matatizo wanayoyakumbanaa nayo wahamiaji hawa iwe mikononi mwa walanguzi au serikali za nchi wanakoelekea Katika mahojiano nami Grace Kaneiya, katika radio ya UM msemaji wa Shirika la Uhamiaji la kimataifa  IOM, Jumbe Omar Jumbe, anaeleza juhudi wanazofanya kuwarejesha wahamiaji hawa nchini mwao.