Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kupoteza chakula ndio kauli mbiu ya siku ya mazingira duniani:UNEP

Kupoteza chakula ndio kauli mbiu ya siku ya mazingira duniani:UNEP

Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP linasema kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya mazingira duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka Juni 5 ni taka za chakula na kupoteza chakula.UNEP inatoa tahadhari kwa suala hilo na upuuzi unaofanyika na kusababisha idadi kubwa ya mazao yaliyozalishwa hayafiki kwa umma kutoka mashambani.

Limeongeza kuwa watu milioni 870 duniani hawana afya inayostahili na wengine kudumaa, na ni tatizo ambalo linafumbiwa macho, hata hivyo kwa mujibu wa shirika la chakula na kilimo FAO kila mwaka tani za chakula bilioni 1.3 kinapotea bure.

FAO inasema idadi hiyo ya chakula kinachopotea ni sawa na kiasi kinachozalishwa na eneo zima la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara.