UNHCR yahmisha wakimbizi wa Darfur kutoka mpaka wa Tissi:

4 Juni 2013

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linaongeza juhudi za kuwapatia maeneo wakimbizi walioko Tissi  ambao sasa wanapatiwa makazi mapya katika kambi iliyopo umbali wa maili chache kutoka mpaka wa Sudan na Jamhuri ya Afrika ya Kati,

Hatua hiyo inachukuliwa ili kukabiliana na tatizo la mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika eneo la Tissi ambalo pia linakabiliwa na hali ya ukosefu wa usalama.

Alice Kariuki anaripoti

(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)

Kwa kipindi cha zaidi ya wiki mbili zilizopita kumekuwa na juhudi za kuwaondosha wakimbizi hao na taarifa zinasema kuwa hadi sasa jumla ya waliohamishwa wamefikia 5,522 .

Kiasi hicho cha wakimbizi ni ongezeko la wakimbizi wengine zaidi ya 1,800 ambao walihamishwa katika kipindi cha mwezi uliopita na kupelekwa katika eneo la Goz Amir.

Tangu May 17 mwaka huu,UNHCR ikiwa na washirika wake, imekuwa na kazi ya kuwatawanya wakimbizi hao kwa wastani wa wakimbizi 500 kila siku ikitumia usafiri wa bara bara.

UNHCR inasema kuwa, inategemea hadi kufikia mwishoni mwa wiki hii, wakimbizi hao wa Tissi watakuwa wamehamishwa kabisa.

Melisa Fleming ni msemaji wa UNHCR

(CLIP YA MELISA FLEMING)