Mjumbe mpya wa UM awasili nchini Somalia
Mjumbe mpya wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Nicholas Kay amewasili nchini Somalia hii leo kuchukua wadhifa wake kama mkuu wa ujumbe wa kisiasa wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia UNSOM.Alipowasili mjumbe huyo wa katibu mkuu amesema amefurahishwa kuwa mjini Mogadishu na kwa kupewa fursa hiyo kuisaidia serikali na watu wa Somalia katika kuleta amani , usalama na kupatikana kwa maendeleo nchini Somalia.
Kay ametoa pongeza nyingi kwa Dr Mahiga na kundi lote na UNPOS akisema kuwa wamekamilisha majukumuyao na wanaweza kujivunia mafanikio waliyoyapata.
Anasema kuwa kile wanacholenga sasa ni uchaguzi wa kitaifa mwaka 2016 akiongeza kuwa changamoto ni nyingi lakini kinachohitajika ni kujitahidi zaidi. Bwana Kay anasema kuwa hivi karibuni atakutana na rais Hassan Sheikh Mohamud na serikali yake na washirika kwenye ujumbe wa AMISOM na IGAD na waashirika wengine wote hususan mashirika ya umma.
Ikiwa ni ofisi mpya ya Umoja wa Mataifa UNSOM ina majukumu ya kuunga mkono jitihada za kupatikana kwa amani kwa lengo la kuwepo uongozi mwema, mabadiliko kwenye sekta ya ulinzi, sheria , haki za bindamu na uwiano.