ILO:Kutokuwepo na uwiano katika upatikanaji ajira ni changamoto

3 Juni 2013

Shirika la kazi duniani, ILO limetoa ripoti yake inayoeleza kuwa  watu zaidi ya Milioni Nane wataingia katika kundi la wasio na ajira katika kipindi cha miaka miwili ijayo na kufanya idadi ya watu wasio na ajira duniani kufikia Milioni 208 . Hii ni kutokana na harakati za kujikwamua kutoka mdororo wa kiuchumi duniani kuendelea kusuasua. Ripoti ya Jason Nyakundi inafafanua zaidi.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Kulingana na ripoti yake ya hivi majuzi kuhusu ajira duniani ILO inasema kuwa nchi zinazoinukia na zinazoendelea zinashuhudia  kuongezeka kwa tatizo la ukosefu wa ajira na mapato kidogo ikilinganishwa na  nchi zilizostawi.Ripoti hiyo hata hivyo inasema kuwa pengo lililopo kati ya matajiri na maskini kwenye nchi maskini na zile za kipato cha wastani linatarajiiwa kuwa kubwa na familia nyingi  ambazo zimejikwamua kutokwa kwenye umaskini zinakabiliwa hatari ya kuporomoka tena.

Raymond Torres ambaye  ni mkurugenzi  wa ILO kwenye taasisi ya kimataifa kuhusu ajira anaeleza baadhi ya changamoto  ambazo zimezuia kuwepo kwa ajira.

(SAUTI YA RAYMOND)

Mikakati mingi hadi sasa imekuwa hatua za muda mfupi kushughulikia hali hiyo  lakini kuna changamoto za muda mrefu ya kurekebisha masuala ya kiuchumi na kijamii.Tukingalia kupitia kwa uchumi ni kwamba faida zimeongezeka lakini uwekezaji bado haijakuwepo kwa kasi. Kuna tofauti kati ya faida na uwekezaji. Kitu kingine muhimu cha kujenga uchumi  na mwanya ulio kati ya makampni makubwa na yale madogo inaonekana kwamba makampuni madogo yanaathiriwa na mzozo wa kiuchumi. Hayana uwezo wa kupata mikopo. Yanakabiliwa na ugumu ya kufika mbali kama makampnui makubwa jambo linaloongeza mwanya  wa kiuchumi