UNAMA imelaani vikali shambulio Mashariki mwa Afghanistan:

3 Juni 2013

Mpango wa Umoja wa Mataifa wa usaidizi nchini Afghanistan UNAMA imelaani vikali mashambulio mawili ya mabomu yaliyofanyika leo Jumatatu Mashariki mwa nchi hiyo na kukatili maisha ya watu 19 wakiwemo watoto zaidi ya 10, yakidhihirisha kwa mara nyingine kuwa wapinzani wa serikali wanalenga maeneo ya raia.Akizungumzia mashambulizi hayo mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa na mkuu wa UNAMA Jan Kubis amesema mashambulizi ya aina hiyo yanasababisha maisha mengi ya watu kupotea huku yakiwa na matunda madogo saana kwa yale waliyokusudia .

Ameongeza kuwa hayakubaliki na hasa yanapotokea kwenye maeneo ya raia. Katika wiki mbili zilizopita machafuko yamesababisha vifo 125 vya raia na kujeruhi wengine 287 ikiwa ni ongezeko la asilimia 24 ikilinganishwa na wakati kama huu 2012.