Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa IAEA yawasilisha ripoti kwa bodi ya magavana:

Mkuu wa IAEA yawasilisha ripoti kwa bodi ya magavana:

Mkurugenzi mkuu wa shirika la kimataifa la nguvu za atomic Yukiya Amano Jumatatu amewasilisha taarifa kwenye bodi ya magavana wa shirika hilo.Katika taarifa hiyo bwana Amano amewaambia nchi wanachama wa IAEA kuhusu masuala ya ukaguzi wa nyuklia ikiwemo nchini Iran na Jamhuri ya kidemokrasia ya watu wa Korea DPRK.

Ametangaza kuwa kongamano la kisayansi la IAEA litakalofanyika Septemba mwaka huu litajikita katika kulinda mazingira ya pwani na bahari.

Pia Bwana Amano ametoa taarifa mpya za ripoti ya shirika hilo kuhusu shughuli zinazoendelea kwenye kinu cha Fukushima Daichi baada ya ajali kwamba zitakamilika mwishoni mwa 2014.