Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muda wa UNPOS wamalizika, UNSOM kuanza majukumu Somalia Juni 3

Muda wa UNPOS wamalizika, UNSOM kuanza majukumu Somalia Juni 3

Muda wa huduma ya Ofisi ya kisiasa ya Umoja wa Mataifa kuhusu Somalia, UNPOS, umemalizika leo, Juni 2. Kuanzia Jumatatu, Juni 3, ujumbe mpya wa Umoja wa Mataifa wa kuisaidia Somalia, UNSOM, utaanza majukumu yake, ambayo ni tofauti na yale yalotekelezwa na UNPOS. Katika taarifa ilotolewa leo, UNPOS imetoa shukrani kwa mchango wa wote walosaidia kufanikisha wajibu wao, na kwa watu wa Somalia na harakati za amani Somalia Akikutana na rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, mjini Yokohama, Japan, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesisitiza ahadi ya Umoja wa Mataifa kuendeleza usaidizi wake imara kwa ajili ya kuikarabati Somalia.  Viongozi hao wawili pia wamezungumza kuhusu majukumu mapya ya ujumbe wa UNSOM, hasa katika kuchangia ofisi bora na kuratibu misaada ya kimataifa, huku Ban akisema wanahohitaji misaada ni lazima waendelee kuipata.