Skip to main content

Ban na Kikwete wajadili albino na mabadiliko ya tabianchi

Ban na Kikwete wajadili albino na mabadiliko ya tabianchi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo amekutana na kufanya

mazungumzo na Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Jamhuri ya Muungano ya

Tanzania, mjini Yokohama, Japan.  Viongozi hao wawili wamezungumza kuhusu hali nchini Madagascar na pia kuhusu haja ya nchi za Afrika kuongea kwa sauti moja kuhusu suala la mabadiliko ya tabianchi.  Mbali na hayo, wamezungumza kuhusu hali ya haki za binadamu za watu wenye ulemavu wa ngozi, yaani albino, nchini Tanzania