Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amos/Pillay wataka raia waruhusiwe kutoka kwa usalama Al-Qusayr inSyria.

Amos/Pillay wataka raia waruhusiwe kutoka kwa usalama Al-Qusayr inSyria.

Mratibu mkuu wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa Valerie Amos na kamishina Mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay wameelezea kusikitishwa kwao na ripoti kwamba maelfu ya raia wamekwama wakati mapigano makali yakiuzingira mji wa Al-Qusayr nchini Syria.

Katik taarifayaoJumamosi maafisa hao wamesema wanatambua kunaweza kuwa na watu takriban 1500 waliojeruhiwa ambao wanahitaji kuhamishwa kwa ajili ya kupata msaada wa haraka wa matibabu na hali kwenye mji wa Al-Qusayr ni mbaya.

Pia wanaendelea kupokea taarifa kwamba makazi ya raia yanaendelea kushambuliwa  na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na sheria za kimataifa unaendelea kutendeka.

Bi Valarie Amos na Navi Pillay wamezitaka pande zote kusitisha mara moja hatua ambazo zitaendelea kukatili maisha ya watu , kuharibu na kuwaruhusu raia kupita kwenda kwenye maeneo yenye  usalama .

Wamezitaka pande zote kukubaliana na usitishaji mapigano  ili kuruhusu wafanyakazi wa misaada kuafirisha majeruhi ma kuwapa msaada unaohitajika.