Skip to main content

Wakuu wa FAO/IFAD na WFP wataka njaa itokomezwe ifikapo 2015:

Wakuu wa FAO/IFAD na WFP wataka njaa itokomezwe ifikapo 2015:

Wakuu wa mashirika matatu ya Umoja wa Mataifa yenye makao yake Roma Italia leo yametoa wito wa kuweka kipaumbele kwenye usalama wa chakula a lishe katika mkutano wa kimataifa wa maendeleo ya Afrika unaoendelea nchini Japan.

Wamesema wakulima wadogowadogo wasaidiwe ili kuimarisha usalama wa chakula na kuwawezesha wanawake, ili kushughulikia siuala la kutokuwepo usawa wa kijinsia na kuwawezesha kubadili maishayao, ya familia zao na jamii zao.

Mkuu wa shirika la chakula na kilimo FAO Jose Graziano da Silva, Rais wa mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo  IFAD Kanayo Nwanze na mkurugenzi mtendaji wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP Ertharin Cousin  wametoa wito huo kwenye mkutano wa kimataifa wa TICAD V Yokohama mjini Tokyo.

Wakuu wa mashirika hayo matatu wamesema njia muafaka ya kutokomeza njaa na kumaliza umasikini katika nchi zinazoendelea ni uwekezaji wa serikali na sekta binafsi katika kilimo endelevu na maendeleo kijijini wakibaini kwamba pato lato la taifa katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara litokanalo na kilimo ni kubwa na linaweza kupunguza umasikini mara kumi na moja zaidi ya sekta zingine.

Wamesisitiza kwamba ni wakati sasa wa kuwekeza katika mabadiliko kwa kuwasaidia wazalishaji wadogo na msahirika yao, kilimo katika familia, wavuvi, wafugaji, wanamisitu, wafanyakazi wa vijijini , wajasilia mali na watu wa asili.