Lazima tushughulikie uhusiano baiana ya amani, usalama na maendeleo Afrika:Ban

2 Juni 2013

Afrika imepiga hatua kubwa katika kufikia malengo ya maendeleo ya milenia MDG’s, lakini mamilioni ya Waafrika, bado hawana ajira,huduma za afya na chakula, huku mamilioni wakipata dhiki kutokana na vita.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon Jumamosi akifungua mkutano wa tano wa kimataifa kuhusu maendeleo barani Afrika TICADV mjiniTokyoJapan.

Ban amesema ili kupata suluhu ya kudumu lazima uhusiano baina ya masuala hayo matatu ushughulikiwe.Ameongeza kuwa kwa kupitia majadiliano kutakuwa na mtazamo wa kimataifa kuhusu uchumi, kijamii na muundo wa mazingira endelevu

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

“Ni vikwazo tunavyopaswa kuvishughulikia kwenye mkutano wa TICAD.Kwanzauchumi, tunahitaji kukuza fursa za biashara za Afrika, uwekezaji mkubwa wenye kuzaa matunda na fursa za utajiri. Pili kijamii,tukuze elimu, afya na kuwawezesha wanawake, na kuthamini uwezo waq vijana wa Afrika. Na tatu kimazingira , mabadiliko ya hali ya hewa yanaathiri mamilioni ya Waafrika. Nchi za Afrika hazijachangoa pakubwa tatizo hili lakini watahitaji msaada zaidi kukabiliana na athari zake”

 Katibu Mkuu Ban amesema ndio maana anafanya kila awezalo kupatikana mkataba wa kimataifa, na kisheria wa mabadiliko ya hali ya hewa ifikapo 2015. Wakati huohuo amesema tunaweza kubadili tatizo la mabadiliko ya hali ya hewa kuwa fursa kwa kutambua umuhimu wa Afrika kwa hewasafi.