Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IAEA yahitimisha mafunzo ya nyukilia Japan

IAEA yahitimisha mafunzo ya nyukilia Japan

Wataalamu wa shirika la Umoja wa Mataifa la nguvu za Atomiki IAEA, wamehitimisha mafunzo ya siku nne yaliyowajengea uwezo wawakilishi kutoka sehemu mbalimbali waliokutana Fukushima Japan.

Zaidi ya washiriki 40 kutoka mataifa 18 wameshiriki mafunzo hayo ambayo pia yalitoa fursa kwa washiriki hao kutembelea na maeneo yaliyokumbwa na tukio la March 2011 wakati vinu kadhaa vya nyuklia vya Japan vilipokuwa kwenye wakati mgumu.

Wakati wa mafunzo hayo, washiriki walijifunza namna ya kukabiliana na mionzi ya nyuklia pamoja na kufanya tathmini ya mazingira.

Afisa mmoja wa wakala wa atomiki Pat Kenny, alisema kuwa mafunzo hayo yametoa fursa muhimu kwa washiriki kujizoesha namna ya kukabiliana na hali hatarishi inayoweza kujitokeza