UNECE yaisaidia Georgia kubuni sheria mpya kuhusu maji

31 Mei 2013

Kipengee kipya cha sheria kuhusu maji kimewasilishwa mbele ya kamati inayoongoza mazunguzo kuhusu sera nchini Georgia inayohusu usimamizi wa maji kwenye mkutano ulioandaliwa mjini Tbilisi tarehe 30 mwezi huu unaoungwa mkono na tume ya Umoja wa Mtaifa kuhusu uchumi barani ulaya UNECE.

Majadiliano na washikadau kuhusu kipengee hicho cha sheria yatafanyika ili kupata majibu. Sheria mpya kuhusu maji inatarajiwa kuanza kutekelezwa ifikapo mwaka 2014 na kuleta mabadiliko makubwa kuhusu usimamizi wa maji nchini Georgia. Ushikiano wa maji kati ya zaidi ya nchi moja pia ulizungumziwa hasa mkutano wa hivi majuzi kati ya Georgia na Azerbaijan kuhusu usimizi wa maji yanayotumika kati ya nchi hizo kwenye bonde la Kura.