Watu zaidi waambukizwa mafuya ya H7N9 China:WHO

29 Mei 2013

Tume ya taifa ya afya na uzazi wa mpango nchini Uchina imeliarifu Shirika la afya duniani WHO kuhusu kuthibitishwa kwa visa zaidi vya virusi vya mafua ya avian H7N9 kwa binadamu.

Tume inasema muathirika wa safari hii ni mvulana wa miaka 6 kutoka Beijing ambaye alianza kuumwa Mai 21 mwaka huu, na kwamba ahali yake kwa sasa inaendelea vyema. Hadi sasa WHO imeaarifiwa jumla ya visa 132 vilivyothibitishwa kwenye maabara vikiwemo vifo 37.

Kwa mujibu wa serikali ya China viongozi katika maeneo yaliyoathirika wanaendelea kufuatilia na kuchunguza na kufanya vipimo mara kwa mara, ikiwa ni panmoja na kuchukua hatua za kuzuia na kudhibiti kusambaa kwa virusi hivyo.

Miji na majimbo yameaanza kufanya operesheni za dharura kuwa za kawaida katika kukabiliana na mlipuko wa mafua hayo. Hadi sasa kwa mujibu wa WHO hakuna ushahidi unaothibitisha maambukizi ya moja kwa moja kutoka kwa binadamu hadi mwingine.

WHO haishauri watu kufanyiwa vipimo maalumu wanapotoka na kuingia Uchina na haishauri marufuku yoyote ya kusafiri kwenda nchini humo.