Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yataka matangazo ya bidhaa za tumbaku kupigwa marufuku

WHO yataka matangazo ya bidhaa za tumbaku kupigwa marufuku

Shirika la afya duniani WHO limetaka mataifa yote duniani kupiga marufuku matangazo yote ya biashara ya tumbaku kama njia mojawapo ya kupunguza idadi ya wavutaji wapya wa tumbaku. Taarifa ya Jason Nyakundi inafafanua zaidi. (RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

WHO inasema kuwa nchi ambazo tayari zimetekeleza marufuku ya matangazo na udhamini kwa bidhaa za tumbaku zimeshuhudia kupungua mwa matumizi ya tumbaku kwa asilimia saba.

Nchi ambazo zimepiga marufuku matangazo ya bidhaa za tumbaku ni pamoja naAustralia,Canada,Finland,Ireland,Nepal,New Zealand,Norway,PalaunaPanama.

Kabla ya maadhimisho ya siku ya kupinga matumzi ya tumbaku duniani ambayo ni tarehe 31 mwezi huu WHO inasema kuwa sekta ya tumbaku inatafuta mbinu tofauti za kulenga wavutaji sigara kupitia kwa mitandao  ya mawasilino  au kwa kutumia wafanyikazi wa makampuni ya tumbaku wanaojifanya kuwa wavutaji sigara. Dr Douglas Bettcher, ni mkurugenzi katika idara ya kuzuia magonjwa yasiyoambukiza kwenye Shirika la WHO

 “Marufuku kwa aina  zote za matanagazo na udhamini  ni moja ya njia kuu ya kupunguza matumizi ya tumbaku. Ukipiga marufu aina moja ya matangazo hasa matatangazo yaliyo maarufu, mabango, kwa njia ya runinga na radio wanageukia mbinu zingine, wakidhamini michezo na  warsha za kijamii. Tunataka kufanya hili kwa kuwa utafiti unaonyesha wazi kuwa theluthi moja ya vijana wanaojaribu kutumia bidhaa za tumbaku hutokana na matangazo na ufadhili. Watumiaji wengi wa tumbaku huanaza kuitumia kabla ya kuhitimu  mika 20 na hakuna shaka kuwa sigara ni dawa unayoua na inayohitaij kupigwa marufuku kwa matangazo yote ya biashara na udhamini ndiyo njia pekee.”

WHO inasema kuwa matumizi ya tumbaku husababisha vifo vya watu milioni 6 kila mwaka.