Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Argentina na hatua za kukinga watoto wa kike dhidi ya kansa ya kizazi

Argentina na hatua za kukinga watoto wa kike dhidi ya kansa ya kizazi

Nchini Argentina, utoaji wa chanjo dhidi ya kirusi cha Human Papillomavirus, HPV kwa watoto wa kike kuanzia umri wa miaka 11 ili kuhakikisha pindi wanapobalehe wanakuwa tayari wameshapatiwa kinga dhidi ya kirusi hicho kinachosababisha kansa ya kizazi. Mpango huo uliopendekezwa na pia kuungwa mkono na shirika la afya duniani, WHO umekuwa wa mafanikio katika nchi hiyo ambayo utoaji wa chanjo yoyote haungalii hadhi ya mtu katika jamii bali kila mtu ana haki ya kupatiwa chanjo ili kuepusha magonjwa. Mkuu wa ofisi ya WHO kanda ya Amerika, Pier Paolo Balladeli amesema wanatumia ili kuhakikisha kila mtoto wa kike anapata chanjo hiyo hususan maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo ambako kiwango cha ugonjwa wa kansa ya kizazi ni cha juu. Argentina ilijumuisha chanjo ya HPV katika mpango wa kitafai mwaka 2011 ambapo watoto wa kike huchanjwa mara tatu na katika miaka miwili ya mwazoni dozi ya kwanza imeshafikia asiilmia 80, dozi ya pili asilimia 60 na dozi ya tatu asilimia 50. Kirusi aina ya HPV husababisha zaidi ya wagonjwa wapya Elfu Tatu kila mwaka wa kansa ya kizazi nchini Argentina na kati yao Elfu Moja Mia Nane hufariki dunia.