Kushiriki ulinzi wa amani kulibadilisha maisha yangu: Insp. Kaneng Muro

29 Mei 2013

Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani leo Mei 29, tumezungumza na baadhi ya watu ambao wamejitolea kutoa huduma hiyo muhimu. Baadhi ya mambo tunayoangazia ni majukumu yao, walivyoitikia wajibu huo, changamoto walizokumbana nazo, na jinsi kuhudumu kama walinda amani kulivyobadilisha mtazamo na maisha yao.

Katika mahojiano yafuatayo, Joshua Mmali amezungumza na Inspekta Kaneng Muro, kutoka jeshi la Polisi Tanzania, ambaye amehudumu UNAMID kuanzia Machi 2010 hadi Machi 2013, na kwanza kumuuliza alihisi vipi pale alipojua kwamba amepata fursa ya kwenda kuhudumu katika ujumbe wa kulinda amani kwenye eneo la Darfur nchini Sudan.