Shirika la UNHCR limewasilisha misaada jimbo la Homs,Syria

28 Mei 2013

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeendesha juhudi za dharura kuwasambazia misaada waathirika wa mapigano yanayoendelea nchiniSyriawaliokwama katika jimbo la Homs.Alice Kariuki anaarifu.(RIPOTI YA ALICE KARIUKI)

Katika kipindi cha mwisho wa juma shirika hilo lilisambaza misaada mbalimbali ikiwemo mablanketi, pamoja na mahitaji mengine muhimu kwa familia zaidi ya 200 ambazo zimeathiriwa na mapigano hayo.

Hapo jana lori la shirikahilolilikiwa limebeba misaada ya usamaria mwema liliwasili katika mji wa Al Wa’er tayari kuwa kusambaza misaada muhimu kwa familia zinazokadiriwa kufikia 10,000.

Eneo hilo linakadiriwa kuwa na wakazi wapatao 400,000 ambao nusuyaowanaishi bila makazi maalumu baada ya kukimbia huko wakitokea katika maeneo mengine ikiwemo wale waliotoka katika mji wa Baba Amer .

Kumekuwa na ongezeko kubwa la wananchi wanaokosa makazi kutokana na mapigano hayo ambayo pia yamesababisha idadi kubwa ya raia kupoteza maisha.