Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNESCO yalaani mauaji ya mwandishi DRC na kutaka kufanyika uchunguzi

UNESCO yalaani mauaji ya mwandishi DRC na kutaka kufanyika uchunguzi

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na elimu, sayansi na Utamaduni ameitaka serikali ya Jamhuri ya Demokrasi ya Congo kuanzisha uchunguzi mara moja dhdi ya mauwaji ya mwandishi wa habari Guylain Chanjabo.Irina Bokova pamoja na kulaani tukio hilo lakini pia ametaka wahusika wa mauwaji ya mwandishi huyo kusaka na kufikiwa chini ya mkono wa sheria.

Mwandishi wa habari Bwana Chanjabo alikuwa akiendesha kipindi kimoja cha redio kilichokuwa kikiendeshwa kwa lugha ya Kiswahili.

Taarifa za kupotea kwake zilianza kusambaa May 5 mwaka huu na baadaye May 17 alikutwa ameokotwa kando kando yam to Ngezi huku akiwa na majeraha kwenye shingo yake.