Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM na serikali ya Uganda kukabiliana na usafirishaji haramu wa watu

IOM na serikali ya Uganda kukabiliana na usafirishaji haramu wa watu

Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, IOM likishirikiana na serikali ya Uganda, limekamilisha warsha ya siku tatu kusaidia kubuni mkakati wa kitaifa wa kukabiliana na usafirishaji haramu wa watu. Mkakati huo utasaidia katika juhudi za kupiga vita uhalifu huo siku zijazo, kwa kutumia msingi ulowekwa na juhudi za sasa. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM (CLIP YA JUMBE OMARI JUMBE)