Mahitaji ya kibinadamu ni makubwa nchini Mali: OCHA

28 Mei 2013

Ofisi ya kuratibu masuala ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa OCHA inasema kuwa kuna mahitaji makubwa ya huduma za kibinadamu eneo la Gao nchini Mali  ambapo viwango vya cha maji ya kunywa vinavyopatikana vimepungua kwa zaidi ya asilimia 60 kwa muda wa majuma machache yaliyopita.

OCHA inasema kuwa ukaratabati wa dharura kwenye mifumo ya maji inahitajika ili kuweza kuwafikishia maji karibu watu 70,000. Ukosefu huo wa maji umetajwa kuwa  huenda ukawa  tisho la mikurupuko ya magonjwa ambapo tayari visa 22 vya ugonjwa ugonjwa wa kipindupindu vimeripotiwa tangu mwanzo wa mwaka huu na vifo viwili vinavyotokana na ukosefu wa maji safi ya kunywa.

Zaidi ya watu 300,000 wanaripotiwa kuhama  makwao nchiniMali. Yens Laerke ni msemaji wa OCHA

(SAUTI YA YENS LAERKE)