Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi Afrika waunga mkono Global Fund kukapambana na maradhi

Viongozi Afrika waunga mkono Global Fund kukapambana na maradhi

Viongozi wan chi mbalimbali za Afrika wametoa wito kwa washirikao wao konte ulimwenguni kuunga mkono juhudi za kuchangisha fedha za fuko la kimtaifa la kupambana na ukimwi, kifua kikuu na malaria yaani Global Fund.

Ombi hilolimetolewa kwenye mkutano wa muungano wa Afrika (AU) mjiniAddis AbabaEthiopiawakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya muungano huo.

Mwenyekiti wa AU waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn, amewataka zaidi ya marais 30 kumuomba kila mtu kusaidia kufanikisha azma ya Global Fund ya kutaka kuchangisha  dola bilioni 15 billion .

Katika azimio lililopitishwa Jumatatu wakuu wa nchi wa Afrika wamesema wanaungana pamoja katika juhudi zao za kupambana na ukimwi, kifua kikuu na malaria.