Ban ahamasisha amani Ukanda wa Maziwa Makuu

24 Mei 2013

Wiki hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon alikuwa na ziara katika Ukanda wa Maziwa Makuu barani Afrika ambapo pamoja na mambo mengine alichagiza mchakato wa amani MAshariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC kufuatia kutiwa saini kwa mkakati wa amani na usalama kwa ajili ya DRC mwezi Februari mwaka huu huko Addis Ababa, Ethiopia. Nchi Kumi na Moja zilitia saini ambapo tayari utekelezaji umeanza huku Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likiwa limeupatia ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC mamlaka mpya ili kuhakikisha ulinzi wa raia. Je ni yapi yaliyojiri? Ungana na Grace Kaneiya katika makala haya.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter