Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bosnia na Herzegovina zinapaswa kutukuza utamaduni: Mtaalamu wa UM

Bosnia na Herzegovina zinapaswa kutukuza utamaduni: Mtaalamu wa UM

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki za kiutamaduni , Farida Shaheed leo amezitolewa mwito serikali zote mbili Bosnia na Herzegovina kutumia fursa na nafasi zilizopo kuwawezesha wananchi wao wanajihusisha kikamilifu na masuala ya utamaduni pamoja na michezo.Pia ametaka kuweka mazingira huru ili masuala ya kisiasa na yale yanayohusu mila na tamaduni za kiutaifa hayaingiliani.

Mtaalamu huyo ambaye amehitimisha ziara yake nchini humo  amelaumu juu ya kile alichokiita siasa  kuteka  mijadala inayohusu  utamaduni na elimu.