Mkutano wa matumizi ya Nuklia kufanyika mwezi ujao Saint Petersburg

24 Mei 2013

Mawaziri kutoka sehemu mbalimbali duniani pamoja na wataalamu wa kimataifa wanatazamiwa kukutana mwezi ujao kwa ajili ya kujadilia hatma ya nguvu za nuklia katika karne hii ya 21, wakati watapokutana kwenye mkutano wa kilele unaoratibiwa na wakala wa Umoja wa Mataifa wa nguvu za atomiki.

Mkutano huo uliopangwa kufanyika kuanzia June 27 hadi 29 hukoSaint Petersburg nchini Urusi unatazamia kutoa mwelekeo muhimu kuhusiana na matumizi ya teknolojia ya nuklia.

Pamoja na mambo mengine mkutano huo pia utatoa fursa kwa watunga serra pamoja na wataalamu kujadiliana namna dunia inavyoweza kuweka zingatio la kuwa na maendeleo endeleo juu ya matumizi ya teknolojia ya nuklia.

Taarifa ilitolewa mjiniViennaimesema kuwa mada kubwa zitakazozingatiwa wakati wa mkutano huo ni kuhusu kuendelea na utumiaji wa teknolojia ya nukilia kwa ajili ya kuzalisha nishati ya umeme lakini kwa tahadhari ya mabadiliko ya tabia nchi.