Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hofu yazidi kutanda wakati M23 wakikabiliana na vikosi vya serikali huko Goma

Hofu yazidi kutanda wakati M23 wakikabiliana na vikosi vya serikali huko Goma

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu linasema kuwa mapigano mapya kati ya vikosi vya serikali na waasi wa M23 huko Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini yameibua hofu kubwakamaanavyoripoti George Njogopa. (RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Mratibu wa masuala ya kiutu Moustapha Soumaré amezitaka pande zote mbili kuheshimu matakwa ya sheria za kimataifa katika wakati ambapo ripoti zinasema kuwa raia watatu waliuwawa kwenye mapigano hayo huku wengine 14 wakijeruhiwa.

Guruneti lilitupwa  katika eneo lijulikanano Ndosha ambalo lipo kazini Magharibi wa mji wa Goma liliuwa watu watatu na kuacha wengine kumi wakiwa wamejeruhiwa vibaya.

Mlipuko huo ambao ulitokea karibu na maeneo yalipo makanisa umesababisha hali ya taharuki kwa mamia ya raia ambao baadhiyaowalilazimika kukimbilia mjini Goma kwa ajili ya kunusuru maishayao.

Yens Laerke ni msemaji wa OCHA

(CLIP YA YENS LAERKE)

Mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa ikiwemo shirika la mpango wa chakula duniani WFP,limesema kuwa kumekuwa na hali ya utulivu kiasi katika baadhi ya maeneo ya mji wa Goma, hatua iliyotoa mwanga kufanikisha zoezi la usambazaji wa mahitaji muhimu kwa wale waliokosa makwao.