WFP Yatoa ripoti ya mpango wa ulishaji chakula mashuleni duniani

24 Mei 2013

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP kwa mara ya kwanza linatoa ripoti inayotanabaisha mpango wa ulishaji chakula mashuleni duniani kotekamainavyoeleza ripoti ya Grace Kaneiya. (RIPOTI YA GRACE KANEIYA)

Ripoti ya hali ya programu ya lishe kwa watoto shuleni  duniani imezinduliwa leo na  WFP, ili kutoa kwa mara ya kwanza taswira na uchambuzi wa programu hiyo katika mataifa yaliyostawi na vile vile yale yanaoendelea , lakini pia ratiba ya jinsi serikali inavyotumia programu ya lishe shuleni kama mazingira bora wakati wa mizozo.

Kwa mujibu wa utafiti, ulioangalia watoto milioni 368, mtoto mmoja kati ya kila watano hupata chakula shuleni kila siku katika nchi 169 zinazoendelea na zile  zilizostawi.

Uwekezaji wa mataifa katika programu hii ni dola bilioni 75 za marekani huku kiwango kikubwa kikitoka kwenye bajeti za serikali.

Hata hivyo kiwango cha programu ya utoaji wa lishe ni cha chini kabisa kule inakohitajika zaidi.

Katika mataifa maskini , ambako watoto wako katika hatari ya umaskini na njaa, ni asilimia 18% tu ambao wanapokea chakula kila siku shuleni ikilinganishwa na asilimia 49% ya watoto katika nchi za kipato kiwango cha wastani.