Uamuzi wa kufanyika kesi mpya kwa Rais wa zamani Guatemala kwa watia hofu waathirika:UM

24 Mei 2013

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema inatiwa hofu na haki za waathirika kutekelezwa hukoGuatemalabaada ya mahakama kubadili hukumu ya Rais wa zamani wa nchi hiyo .

Rais huyo alihukumiwa kwa mashitaka ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na sasa kesi yake imeamriwa kuanza kusikilizwa upya. Umoja wa Mataifa unasema waathirika wa ukatili huo wamesubiri kwa muda mrefu kupata fidia lakini sasa matumaini hayo ynaonekana kutoweka  baada ya uamuzi huo wa mahakama.

Pia Umoja wa mataifa unatiwa shaka kwamba kusikilizwa upya kwa kesi hiyo kutawaweka mashahidi mahali pabaya zaidi. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)