Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hakuna amani bila maendeleo na hakuna maendeleo bila amani: Ban

Hakuna amani bila maendeleo na hakuna maendeleo bila amani: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon bado yuko ukanda wa maziwa makuu barani Afrika ambapo tayari yukoUgandaakitokeaRwandaakiendeleza ajenda ya amani kwenye eneohilolililogubikwa mzozo ambao umejikita Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC.  Akiwa mjini Kigali, Bwana Ban ambaye anaambatana na Rais wa Benki ya dunia Jim Yong Kim,  alikuwa na mazungumzo na Rais Paul Kagame ambapo baadaye katika mkutano na waandishi wa habari alieleza kuwa mikutanoyaoilikuwa ya manufaa. Mathalani aligusia utekelezaji wa mkakati wa amani na usalama kwa ajili ya DRC ambaoRwandapia imetia saini na kusema kuwa mafanikio iliyo nayoRwandahivi sasa yatadumu iwapo kuna amani ukanda mzima.

 (SAUTI YA BAN)

 “Hakuwezi kuwepo kwa amani bila maendeleo, na hakuna maendeleo bila amani. Rwanda imetoka mbali sana katika miongo miwili. Serikali na wananchi wake wanapaswa kujivunia. Hata hivyo manufaa ya amani ya kudumu yanapaswa kutandaa eneo lote jirani na Rwanda. Mkakati wa amani, usalama na ushirikiano DRC na ukanda wa maziwa makuu ni fursa nzuri ya amani kwa miaka mingi ijayo.

Halikadhalika Bwana Ban alipongeza vileRwandakatika miongo miwili imesonga mbele na hata kuwa katika mwelekeo mzuri wa kufikia malengo ya maendeleo ya milenia ikiwemo kutokomeza umaskini na usawa wa jinsia.