Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Twahitaji wataalamu zaidi wa kutibu Fistula: CCBR

Twahitaji wataalamu zaidi wa kutibu Fistula: CCBR

Wakati dunia inaadhimisha siku ya kwanza kabisa ya kutokomeza Fistula, jeraha alipatalo mzazi wakati wa kujifungua iwapo anakosa huduma muhimu au maungo yake hayajakomaa kubeba ujauzito, hospitali ya CCBRT nchiniTanzaniainasema bado wataalamu hawatoshi kukidhi mahitaji wakati huu ambapo elimu zaidi inatolewa ili wanawake wenye Fistula waweze kujitokeza kutibiwa jerahahilo. Kauli hiyo ni ya Dokta Robert Marenga, mtaalamu wa kutibu Fistula kwenye hospitali ya CCBRT na alitoa alipohojiwa na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa jijini DSM. Kwanza Dokta Marenga anaanza kwa kueleza tiba wanayotoa.