Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tulifeli Rwanda lakini tuzuie baa linalojitokeza Syria: Ban

Tulifeli Rwanda lakini tuzuie baa linalojitokeza Syria: Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuungana kuzuia baa linalojitokeza nchini Syria, hata ingawa ilishindwa kuzuia mauaji ya kimbari nchini Rwanda.Bwana Ban amesema hayo mjini Kigali, Rwanda, wakati akizuru tena eneo la kaburi la halaiki na kumbukumbu ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

Bwana Ban amesema kaburi hilo la kumbukumbu ni muhimu kuukumbusha ulimwengu kuwa usiwahi kusahau unyama unaoweza kuzuka kwenye mioyo ya wanadamu, na kuongeza kuwa ni lazima kuwepo tahadhari wakati wote.

 Bwana Ban amesema kaburi la kumbukumbu ya mauaji ya Rwanda ni onyo na ishara ya matumaini, na kuwapongeza watu wa Rwanda kwa kuridhiana na kujikwamua tena, chini ya miongo miwili.