Ukame ni janga linaloongezeka Pembe ya Afrika:

23 Mei 2013

Geneva, Uswisi kunafanyika mkutano wa kudhibiti au kupunguza athari zitokanazo na majanga na leo tunaangazia pembe ya Afrika. Kwako Alice Kariuki.(RIPOTI YA ALICE)

Hali ya ukame ni janga linaloongezeka kila uchao katika Pembe ya Afrika. Hayo yameelezwa kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa wa upunguzaji majanga unaoendelea mjiniGeneva.  Lakini jinsi gani nchi hizo zinakabiliana na tatizohilo? Mathewos Hunde Tulu ni afisa kutoka shirika la IGAD

(SAUTI YA HUNDE TULU)

Nadhani kuna mikakati kadhaa iliyopo ili kushughulia hatari ya majanga na athari zake. Mikakati imechukuliwakamasehemu ajenda ya maendeleo endelevu.

Nchi nyingi sasa zimetambua kwamba mtazamo mmoja ama kujikita katika kushughulikia sababu tuu au kuboresha hatua za kuchukua baada ya majanga haviwezi kuwa na matunda mazuri, hivyo sasa kuna mtazamo mseto ambao unashughulikia chanzo na kuborosha juhudi za uwezo wa kukabiliana nayo.