Kutokomeza Fistula kutanufaisha jamii -Ban

23 Mei 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametoa ujumbe katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya kutokomeza fistula itokanayo na uzazi na kusema  kutokomeza hali hiyo ya kupata jereha wakati wa kujifungua sio tu kwamba kutasaidia katika kufikia malengo ya maendeleo ya milenia balia pia kutasawasaidia watoto watakaolelewa na mama wenye afya na mchango wao utanufaisha jamii nzima kwa ujumla. Bwana Ban amesema kufikia hilo huruma, kujali pamoja na fedha zinahitajika na kuongeza kuwa ni muhimu kuwasaidia wanawake waliotengwa kutokana na Fistula ili wajiunge tena na jamii zao. Amesema  licha ya kwamba wajawazito wanatazamia muujiza wa kupata watoto ni muhimu pia kukabiliana na ukweli kwamba  mchakato huo ni hatarishi kwa wale ambao hawapati huduma nzuri ya matibabu.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter