Visa vya ugonjwa wa novel Coronavirus vyathibitishwa eneo la maashariki ya kati

23 Mei 2013

Wizara ya afya nchini Saudi Arabia imelifahamisha Shirika la afya duniani WHO kuhusu kuthibitishwa kwa ugonjwa wa kupumua unaofahamika kama Novel coronavirus. Taarifa zaidi na Jason Nyakundi.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Kisa cha ugonjwa huo kiliripotiwa kutoka eneo la Al-Qaseem kati kati mwa nchi na inasemekana kuwa hakina uhusiano na visa vilivyoripitiwa kutoka eneo la Al-Ahsa mashariki mwa nchi. Mgonjwa huyo alilazwa hospitalini akiwa na matatizo ya kupumua tarehe 15 mwezi Mei mwaka huu na kuaga dunia siku tano baadaye.

Uchunguzi kuhusu kuugua kwake unaendelea. Utawala nchini Saidia unaendesha uchunguzi kuhusu mkurupuko kwa ugonjwa huo ambao ulianzia kwenye kituo kimoja cha afya tangu mwanzo wa mwezi Aprili eneo la Ahsa. Hadi sasa jumla ya wagonjwa 22 vikiwemo vifo 10 vimeripotiwa kufutia mkurupuko huo.

Shirika la afya duniani limepokea ripoti za kuthibitishwa kwa visa kadha vya ugonjwa huo kutoka nchini Jordan, Qatar, Saudi Arabia, muungano wa nchi za kirabu, Ufaransa, Ujerumani , Tunisia na Uingereza.

Nchi zote wanachama ziemekumbushwa kulifahamisha shirika la WHO kuhusu visa vyovyote vipya vya ugonjwa wa Novel Coronavirus na pia kuhusu maambukizi yoyote.