Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Benki ya dunia yaahidi dola bilioni 1 kwa ukanda wa Maziwa Makuu

Benki ya dunia yaahidi dola bilioni 1 kwa ukanda wa Maziwa Makuu

Benki ya Dunia imeahidi dola bilioni mojakamamsaada mpya wa fedha kwa ajili ya kusaidia nchi za ukanda wa Maziwa Makuu katika kuboresha huduma za afya, elimu na kukuza biashara miongoni mwa nchi hizo, pamoja na miradi ya kuzalisha umeme. Ahadi hii ya msaada ni kwa lengo la kusaidia mkataba wa amani wa nchi za Maziwa Makuu uliosainiwa na nchi 11 mwezi  Februari mwaka huu, mjiniAddis Ababa.Rais wa Benki ya Dunia   Dr. Jim Yong Kim ambaye ameambatana na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ziarani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, na baadaye Rwanda na Uganda, amesema usalama na maendeleao katika ukanda wa nchi za Maziwa Makuu ni muhimu kwa ajili ya juhudi za Afrika za kupunguza umaskini uliokithiri, na kujenga mafanikio kwa mamilioni ya watu ambao wamekuwa na fursa ndogo za kiuchumi.

Katika hatua nyingine,  Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika ukanada huo, Mary Robinson aliyeambatana na viongozi hao katika ziara hiyo, amewataka watu, serikali ya DRC na jumuiya ya kimataifa  iamini kwamba inawezekana amani ya nchi hiyo kurejeshwa kwa kuwa fursa hiyo ipo, akisisitiza kuwa kuna matumaini na nafasi katika hali hiyo ya sintofahamu.