UM kuzindua stamp za uhifadhi wa bahari

22 Mei 2013

Katika kuadhimisha siku ya kuhifadhi bahari duniani, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya posta UNPA, inatarajia kutoa stempu tatu zilizoandaliwa kwa ajili ya kukuza uelewa kuhusu siku hiyo.

Stamp hizo zinazotarajia kuanza kuuzwa May 31 mwaka huu zitakuwa na taswira zilizobuniwa na mtunzi wa vitabu vya watoto Dk Seuss.

Katika kuendeleza siku ya mabahari UNPA ilishirikiana na kampuni ifahamikayo kama Dk Seuss Enterprises ambapo wahusika katika taswira za stamp wanatoa mtazamo wa kipekee kuhusu afya ya bahari.

Mkurugenzi wa ubunifu kutoka UNPA Rorie Katz amesema ulinzi dhidi ya bahari za dunia ni somo muhimu ambalo linastahili kupokelewa na watu duniani na kusisitiza kwamba ubunifu wa matumizi ya taswira zilizonakshiwa katika stempu utatoa fursa ya kuvutia watu juu ya kuhifadhi bahari .