IAEA kujenga kituo cha kukabili majanga ya dharura Japan

22 Mei 2013

Wakala wa Umoja wa Umoja wa Mataifa wa nguvu za Atomiki umetangaza mpango wa kuipiga jeki serikali ya Japan ili kufanikisha ujenzi wa kituo maalumu katika eneo la Fukushima kwa ajili ya kukabiliana na majanga ya dharura.

Kituo hicho kitatumika kama nyenzo muhimu ya wakala huo kukabiliana na majanga yoyote ya dharura yatayojitokeza nchini Japan na katika maeneo mengine duniani.

Kujengwa kwa kituo hicho kunafuatia hali manusura iliyolikumba eneo la Fukushima kufuatia tetemeko kubwa iliyolikumba Japan ambayo ilisababisha mitambo yake ya nuklia kwa ajili ya kuzalisha umeme kuingia katika dosari.

Sherehe za kukamilisha mipango kwa ajili ya ujenzi wa kituo hicho zimepangwa kufanyika May 27 na baadaye kufuatiwa na warsha maalumu ambayo inatazamiwa kukamilika ifikapo May 31.