Huu ni wakati muhimu sana kwa DRC na eneo la Maziwa Makuu

22 Mei 2013

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

"Lakini makubaliano hayo ni lazima yatafsiriwe kwa vitendo. Muafaka wa amani ni lazima uzae matunda ya amani kwa watu, Dr. Kim na mimi tunasafiri katika eneo hili katika ziara ya kwanza ya aina yake kuonyesha mshikamano na uungaji wetu mkono.Kila mahali tunakokwenda tutawataka viongozi kutimiza wajibu wao".

Ban amesema Rais Kabila anajitahidi kutimiza wajibu wake na amempongeza kwa kuanzisha mkakati wa kitaifa ambao utasaidia utekelezaji wa makubaliano hayo ikiwemo kufanya mabadiliko muhimu, kuwa na majadiliano ya kisiasa na maridhiano. Ban amemuhakikishia Rais Kabila kwamba jumuiya ya kimataifa itakuwa pamoja nao kwani watu wengi saana wameteseka kwa muda mrefu katika taifa hilo.