Zaidi ya watu milioni 7 sasa wanapata matibabu dhidi ya HIV Afrika: UNAIDS

21 Mei 2013

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

 

Wakati Muungano wa nchi za Afrika (AU) unapoanza mkutano wake wa 21 na kuadhimisha miaka 50 ya kuungana kwa bara Afrika, Mpango wa pamoja wa Umoja wa Mataifa kuhusu virusi vya HIV na UKIMWI (UNAIDS), umetoa ripoti mpya inayoonyesha hatua zilizopigwa katika kupiga vita UKIMWI barani humo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, idadi ya watu wanaopokea matibabu ya dawa za kupunguza makali ya virusi vya HIV imeongezeka na kufikia milioni 7.1 mwaka 2012, wakati idadi hiyo ilikuwa chini ya milioni 1 mnamo mwaka 2005. Mwaka uliopita pekee, idadi hiyo ilipanda kwa watu milioni moja.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo ya UNAIDS, vifo kutokana na UKIMWI pia vimeendelea kupungua- viwango vya vifo vikishuka kwa asilimia 32 kati ya 2005 na 2011, huku viwango vya maambukizi mapya ya virusi vya HIV vikishuka kwa asilimia 33 kati ya 2001 na 2011.

Ripoti hiyo inasema ufanisi huu umetokana na uongozi imara na wajibu wa ushirikiano barani Afrika na katika jamii ya kimataifa, huku ikitoa wito kuwepo juhudi endelevu ili kuhakikisha bara Afrika linafikia lengo la kutokomeza maambukizi, ubaguzi na vifo vitokananvyo na UKIMWI.