Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu asikitishwa na janga la huko Oklahoma

Katibu Mkuu asikitishwa na janga la huko Oklahoma

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amewandikia barua Gavana wa jimbo laOklahomanchini Marekani kufuatia janga la vifo na majeruhi lililotokana na tufani iliyopiga eneohilosiku ya Jumatatu. Bwana Ban amesema yeye binafsi na Umoja wa Mataifa kwa ujumla wako pamoja na wakazi wa jimbo hilo na kwamba wako tayari kutoa msaada wowote kadri watakavyoombwa katika kusaidia jitihada za kujikwamua na janga hilo. Katibu Mkuu pia ametuma rambi rambi kwa familia za wafiwa na wote wale walioathiriwa na tufani hiyo.