Sekta thabiti ya kilimo itasaidia kuimarisha afya: AU

21 Mei 2013

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Dkt. Nkosazana Dlamini-Zuma amehutubia baraza la afya la shirika la afya duniani, WHO hukoGeneva, Uswisi na kusema kuwa Umoja wa Afrika unaamini kuwa kuboresha sekta ya kilimo ni njia mojawapo ya kuimarisha sekta ya afya. Dkt. Nkosazana amesema sekta hakika ya kilimo itawezesha kupatikana fedha za ziada kwa ajili ya kuimarisha sekta ya afya. 

(SAUTI YA Dkt. Nkosazana)

 Kupatia kipaumbele kilimo, chakula, lishe na usalama, kwa kuwa na uhakika wa chakula tunaweza kuokoa zaidi ya dola Bilioni Mbili ambazo kwa sasa tunatumia kuagiza chakula. Na tunafirikiri fedha hizi zinaweza kupelekwa kwenye elimu na afya na vipaumbele vingine na wakati huohuo tunaweza kuongeza thamani katika chakula tunachozalisha.”

 Halikadhalika amesema Umoja wa Afrika unaamini katika kutoa elimu dhidi ya mambo yanayochagiza magonjwa yasiyo ya kuambukiza, mathalani kuelimisha watu juu ya madhara ya uvutaji sigara, na hivyo kuwa na jamii yenye afya. Amewaeleza wajumbe pia kuwa suala muhimu ni kuhakikisha marekebisho ya upatiaji fedha sekta ya afya yalenge kuboresha huduma za msingikamanjia mojawapo ya kuimarisha afya ya jamii.