Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yahaha kudhibiti mlipuko wa kipindupindu Niger.

UNHCR yahaha kudhibiti mlipuko wa kipindupindu Niger.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linahaha kudhibiti mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu kwenye kwambi za wakimbizi nchiniNiger, tangu serikali ya nchi itangaze mlipuko wa ugonjwa huo tarehe 11 mwezi huu. Mlipuko wa kipindupindu magharibi mwaNigerhadi sasa umesababisha vifo vya watu Saba wamekufa wakiwemo wakimbizi wawili kutokaMaliwaliokuwa wakiishi kambi ya Mangaize. Melissa Flemming ni msemaji wa UNHCR.

(SAUTI YA MELISSA)

Kipindupindu ni ugonjwa unaosababishwa na kunywa maji machafu hususan yaliyochanganyika na kinyesi kibichi.