Kilio cha makabila asili kisikilizwe :Sena

20 Mei 2013

Mwenyekiti wa Kikao cha 12 cha kudumu cha Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya makabila asili Paul Kanyinke Sena amezitaka serikali kupatia ushirikiano makabila yanayodai haki mbali mbali kwa kuwa makundi hayo nayo yana nafasi katika ujenzi wa nchi zao.

Bwana Sena ameiambia Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani kandoni  mwa kikao na waandishi wa habari kuwa kutosikilizwa kwa makundi hayo kunayanyima fursa akitolea mfano barani Afrika ambapo amesema baadhi ya viongozi hawako tayari kukutana na makundi haya kwa fikra kwamba wanakinzana na serikali zao.

Amesisitiza kwamba lengo la harakati za makabila asili si kujenga uadui bali ni kutambulika na kushiriki katika ujenzi wa nchi zao.

(SAUTI SENA)