Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utayari wa wasomali umerahisisha mchakato wa amani- Balozi Mahiga

Utayari wa wasomali umerahisisha mchakato wa amani- Balozi Mahiga

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  Balozi Augustine Mahiga anahitimisha wadhifa wake huo mapema mwezi ujao baada ya kuhudumu kwa miaka mitatu.Katika kipindi chakeSomaliailiyokuwa imegubikwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kwa zaidi ya miongo miwili imeweza kuwa na serikali, bunge na sasa mchakato wa kujenga miundombinu inaendelea. Katika sehemu hii ya pili ya mahojiano maalum na Assumpta Massoi wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa, Balozi Mahiga anazungumzia kile kilichofanikisha mchakato wa kisiasa.

Balozi Mahiga akihojiwa na Assumpta Massoi, Usikose sehemu ya tatu na ya mwisho wiki ijayo. Je baada yaSomalia, Balozi Mahiga anaelekea wapi? Basi hadi wakati mwingine. Mimi ni Grace Kaneiya, kwaheri kwa sasa.