Ban aipongeza Msumbiji kwa kuwapa wanawake nafasi

20 Mei 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon ambaye yuko ziarani Msumbiji leo amekutana na spika wa bunge la nchi hiyo bi.Veronica Nataniel Macamo Dhlovo.

Amempongeza kwa kuwa mwnamke wa kwanza kushika wadhifa huo nchini Msumbiji na kuongeza kuwa ametiwa moyo na idadi ya wanawake walioko bungeni.

Ban na Bi Macamo wamejadili baadhi ya changamoto kubwa zinazoikabili Msumbiji na kubadilishana mawazo ya jinsi gani Umoja wa Mataifa utaisaidia nchi hiyo kukabili changamoto hizo.

Makamu wa rais, wenyeviti wa tume mbalimbali za bunge na wabunge wa upinzani ni miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo.

Katibu Mkuu amepongeza juhudi za bunge la nchi hiyo kuchagiza mshikamano na majadiliano ya kisiasa ambayo yamesaidia kuimarisha amani Msumbiji.