Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bokova azuru Afghanistan kuchagiza elimu ya mtoto wa kike:UNESCO

Bokova azuru Afghanistan kuchagiza elimu ya mtoto wa kike:UNESCO

Mkurugenzi mkuu wa shirika la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO Bi Irina Bokova ametumia ziara yake nchini Afghanistan kuchagiza kuhusu elimu kwa mtoto wa kike na kueleezea umuhimu wa urithi wa utamaduni wa taifa hilo kama kivutio cha kiuchumi.Katika ziara hiyo ya siku tatu Bi Bokova amekutana na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Rais Hamid Karzai.

Bi  Bokova pia amekutana na wanafunzi na wafanyakazi wa sekta ya utamaduni yaAfghanistanna kumpongeza Rais Karzai kwa kuinua elimu ya motto wa kike, kufuta ujinga na kuendelea kuunga mkono malengo ya UNESCO.

 (CLIP YA IRINA BOKOVA)